Tukio la kuchomwa Moto Maskani ya CCM Kisonge kisiwani  Unguja limesababisha pia mali na baadhi ya Vyombo vilivyokua hapo kuteketea kwa Moto kama inavyoonekana Vespa iliowekwa eneo hilo ambayo mmiliki wake hajajulikana ikiteketea.
 Jeshi la Polisi lilionekana likifanya Doria katika sehemu hio ilikuweka hali ya Usalama.
 Wafanyakazi wa Kikosi cha Zima Moto wakijitahidi kuuzima moto uliokuwa ukiwaka ndani ya Jengo la Maskani ya kisonge lililochomwa moto na watu wanaodaiwa ni wafuasi wa Sheikh Faridi wakisindikiza kuachiwa kwa Sheikh wao huyo ambae wanadhani amekamatwa na Polisi baada ya kutomuana kwa siku Nzima,Jeshi la Polisi limekanusha kumkamata Sheikh huyo na kuwaomba wananchi kushirikiana kumtafuta.
PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR.



TAARIFA YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewataka wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vimedhibiti hali ya  ulinzi na imeimarishwa katika maeneo yote ya Zanzibar.


Taarifa ya Serikali iliyotolewa leo usiku na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed imesema Zanzibar bado ni shwari na inaendelea kuwa katika hali ya amani na utulivu.

Akizungumzia tukio la vurugu zilizofanywa na wananchi wachache, Waziri Mohamed Aboud alisema vikundi vya vijana vinavyosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Sheikh Farid Hadi walifanya vurugu hizo katika mitaa ya Darajani, Michenzani, Muembeladu,Magomeni,Amani wakidai Sheikh wao haonekani na kudhani amekamatwa na vyombo vya Dolan a kuwekwa ndani.

Waziri Mohamed Abud alisema Serikali imewasiliana na vyombo vya Dola ikiwemo Polisi,Jeshi la wananchi wa Tanzania, Idara ya Usalama wa Taifa, Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,KMKM,JKU,Chuo cha Mafunzo,Zimamoto na Valantia ambapo vyombo vyote hivyo vimeeleza kutoelewa chochote kuhusu Sheikh Farid.

Waziri huyo alisema kwamba Jeshi la Polisi limepokea taarifa ya kutoonekana kwa Sheikh Farid  ambapo kwa sasa Jeshi hilo linaendelea kumtafuta na kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ili kupata ukweli wake na kuchukua hatua zinazofaa.

Alisema kwamba wakati Jeshi la Polisi likiendelea na upelelezi wake, wananchi wameombwa kutoa taarifa kuhusu tukio hilo kwa vituo vya Polisi  au kupitia Masheha, Ofisi za Wilaya na Mikoa katika maeneo yao.

Waziri Mohamed Aboud amesema Serikali inawasihi wwananchi  waache kujiingiza katika vitendo vya fujo na vurugu kwani kutenda hivyo ni kosa kwa mujibu wa sheria na Serikali haitovumilia vitendo hivyo.

Katika tukio la leo mchana, vijana hao wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Sheikh Farid Hadi walifanya vitendo vya vurugu ikiwemo kuchoma moto Maskazini za CCM,kuvunja maduka,kupora mali za watu na kuharibu miundombinu ya barabara na kusababisha hasara kubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Du kali hii

    ReplyDelete
  2. Ndugu zenu munawaelewa vizuri lakini munawawachia kufanya uharibifu kama huu kwa visingizio vya uamsho.

    Hao wanaojiita mbwa wa mwitu na ubaya ubaya kwa nini munawafumbia macho kufanya vitendo vya kinyama kama hivi?

    ReplyDelete
  3. zanzibar hamna shwari wala hakutokuwa na shwari serikali ya mapinduzi na ile ya muungano ni vema wakakaa kitako na kufanya mageuzi ya siasa kuhusu muundo wa muungano na kuacha dhana ya kufikiri nguvu au babaisha bwege ya katiba na sensa na visingizio vingine kuwa ndio nchi itakuwa shwari,mageuzi tanzania kama kufa na kiumbe kwa sasa muda wa kuyazuia ni sawa na kuzuia sunani kwa waya wa kuchujia nazi.
    ushauri wangu wa bure kwa taifa letu kuweni wepesi wa kuona yale yasioepukika badala ya kuwa vipofu japokuwa mna mawani ya kila rangi sheikh farid inawezekana amelala kwake kwa mke mdogo na wale wake zake wawili hawajui kwani ana watoto ishirini na umri wake si zaidi ya miaka 35 sasa msiuwane bure mtafuteni kwa wake zake kwanza wote watatu tunaowajua sisi au kama ameongeza wa nne kwa mujibu wa dini hilo pia mlichunguze kwani isije kuwa amelala zamu nyumba mpya huku vijana wake wanabomoa maskani na kharibu mali za watu.
    uwezekano wa kuwa yupo gerezani mwanza au shinyanga huo upo pia kwani zamani hayo yalitendeka hapa zanzibar baadhi ya wafungwa waliambiwa wanenda kuchuma maembe tumbatu wakaja shitukia wako bagamoyo njiani kuelekea magereza ya bukoba na kigoma kwa hiyo huyu sheikh asiombe akawa yuko huko ni heri awe kalala kwa mke mdogo.
    mdau.
    mirembe hospital,dodoma.

    ReplyDelete
  4. Si wezi kuamini kuwa Serikali ya mapinduzi zanzibar na vyombo vyake vya ulinzi na usalama vimeshindwa kudhibiti hizi vurugu za mara kwa mara. siku za nyuma walikuwa wanatupa mawe, majuzijuzi wamechima maskani ya CCM pale rahaleo, baada ya kuona wameendelea kuachiwa bila ya udhibiti sasa wamechoma nyengine hapo kisonge na kuua askari, na kwa haya wataachiwa...what next?

    ReplyDelete
  5. Waislamu Zanzibar mtatueleza Sheikh yuko wapi kwa siku ya 5 sasa,

    Angalieni leo Ijumaa tunaswali peke yetu kwenye Mimbar Hotuba atatoa nani Sheikh hayupo?

    Kama sivyo tutaunguza hadi aridhi pia!

    ReplyDelete
  6. Unguza unguza hii ndio muone Libeneke la Uislamu wetu sisi Uamsho!

    ReplyDelete
  7. Mdau wa tatu Fri Oct 19, 02:56:00 AM 2012

    Hahahahaha!

    Unanichekesha kwa mwanaume miaka 35 tu?, sema hata kama angekuwa ana zaidi ya 65 inawezekana akawa anajisikia akiwa na wake wawili 2 anaweka akavuta wa tatu !

    Kuzeeka kwa mwanaume ni pale jogoo litakapokuwa uwezo wa kuwika umeshuka au umekufa kabisa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...