Kaimu Mkurugenzi na Muendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Dkt. Kanael Nnko (wa pili kutoka kulia) akiwakabidhi vyeti wahitimu wa mafunzo Yya wataalamu wa Taasisi za fedha zilizoshiriki.

BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia BoT Academy leo Mei 03, 2024  imefunga mafunzo kwa wataalamu 52 kutoka Benki washirika kuhusu namna bora kutoa mikopo katika sekta ya kilimo pamoja na kuangalia viatarishi jambo ambalo litasaidia taasisi za fedha kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta tija kwa Taifa.

Mafunzo hayo yameendeshwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia Madi wa BoT Academy kwa lengo la kuzalisha wataalamu wengi katika taasisi za fedha ambao watasaidia kutoa mikopo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo hayo,  Kaimu Mkurugenzi na Muendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Dkt. Kanael Nnko, amesema kuwa mafunzo yatakwenda kuleta tija katika utoaji wa mikopo sekta ya kilimo.

Dkt. Nnko amesema kuwa lengo ni kuhakikisha idadi kubwa ya wakulima wanafikiwa na kupata mikopo katika Mikoa yote kwa maendeleo ya Taifa.

“Tunaamini mafunzo haya pamoja na washiriki yanakwenda kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu yetu ya hakikisha sekta ya kilimo inasonga mbele” amesema Dkt. Nnko.

Amesema kuwa TADB katika kipindi cha miaka sita mpaka sasa mfuko wa dhamana wa Benki ya Kilimo umeweza kudhamini mikopo ya shilingi bilioni 270 kupitia benki washirika.

Ameeleza kuwa wameweza kuwafikia wakulima walengwa 24,000, huku benki ya washirika wametoa asilimia 11 ya mkopo katika sekta ya kilimo na kuendelea kuongeza juhudi ili kufikia mwaka 2030 sekta ya mikopo ili imefika asilimia 30.

“Kilimo ni sekta kubwa hivyo huwezi kuwafikia wote kwa siku moja, juhudi zinaendelea kufanyika ili vijana, wakina mama na baba waweze kuingia katika sekta ya kilimo” amesema.

Amefafanua kuwa mafunzo hayo yameendeshwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia BoT Academy pamoja na washirika wengine kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) pamoja na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) na chuo cha Benki Kuu Mwanza  ambao wameshiriki katika kuunda mifumo pamoja na kufundisha.

Makamu wa Mkuu wa Chuo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dkt. Ephraim Mwasanguti, amesema kuwa miongoni mwa majukumu yao ni kutoa elimu kwa mabenki na taasisi za fedha kuhusu utekelezaji wa majukumu mbalimbali.

Dkt. Mwasanguti amesema kuwa lengo la mafunzo ni kutoa elimu kwa maafisa wa mikopo ili waweze kutoa mikopo ambayo italipika na kuleta matokeo chanya katika sekta ya kilimo.

“Tulipewa kazi na benki ya maendeleo ya kilimo ya kutengeneza programu kwa ajili ya wakulima wadogo wadogo hasa ikilenga kuelimisha mabenki hasa maafisa mikopo ili waweze kutoa mikopo ambayo italipika kwa sababu hizi ni fedha za umma na kuleta matokeo mazuri katika nchi yetu” amesema Dkt. Mwasanguti.

Nao baadhi ya wahitimu wakiwemo Meneja Mahusiano Kitengo cha wateja wakubwa ABSA Benki, Mollen Charles pamoja na Meneja Uhusiano Kilimo Biashara Benki ya CRDB Salvatory Sylvester, wamesema kuwa mafunzo hayo yanakwenda kuwasaidia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa.
Kaimu Mkurugenzi na Muendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Dkt. Kanael Nnko akizungumza jambo katika hafla ya kufunga mafunzo ya Wataalam kutoka Benki washirika kuhusu namna bora kutoa mikopo katika sekta ya kilimo iliyofanyika leo Mei 3, 2024 katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliyopo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Mkuu wa Chuo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dkt. Ephraim Mwasanguti akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kutoa mafunzo kwa wataalam kutoka Benki washirika kuhusu namna bora ya kutoa mikopo katika sekta ya kilimo.
Meneja Mahusiano Kitengo cha wateja wakubwa Benki ya ABSA Mollen Charles akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa mafunzo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Meneja Uhusiano Kilimo Biashara Benki ya CRDB Salvatory Sylvester akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa mafunzo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
    
MERIDIANBET Kasino ya Mtandaoni kuna shindano la Expanse ambalo mwanzo maokoto yalikuwa mengi lakini, Bosi kacheka ameamua kuongeza pesa na sasa kuna jumla ya Shilingi Milioni mia nne, bonasi za kasino, mizunguko na beti za bure. Jisajili Meridianbet usipitwe na Promosheni hii.

Mtoa huduma wa michezo ya kasino ya mtandaoni Expanse Studio anashirikiana na Meridianbet kuwaletea shindano kubwa la zawadi, mgao wa Mamilioni unakusubiri, kwa kucheza michezo ya sloti na kasino unajiweka kwenye nafasi ya kushinda, dau la kuanzia ni Tsh 400/=

Kanuni za Shindano la Expanse Kasino ya Mtandaoni

Promosheni hii imeanza 04.05. 2024 hadi Mei 17 ambapo bonasi za kasino zitagawiwa kwa washindi watakaokuwa wanatangazwa kila siku, baada ya kucheza moja kati ya michezo ya kasino ya mtandaoni iliyopo Meridianbet kutoka Expanse studio.

Promosheni ni halali kwa wachezaji waliosajiliwa kwenye APP na tovuti ya meridianbet.co.tz

Promosheni itafanyika katika mtindo wa mashindano kwa wachezaji kwenye sloti zinazotolewa na Expanse Studio. Michezo ya kasino ya mtandaoni itakayotumika wakati wa promosheni ni:

Battle of Egypt
Forest Rock
Fortune Farm
Lucky's Betting Shop
Maya's Treasure
Piggy Party
Spinning Buddha
Sticky 777
The Book of Eskimo
Veni Vidi Vici
Wild Corrida
Zombie Apocalypse
Battle for the Throne
Bounty Hunters
Capital City Derby
Casino Heist
Fairy in Wonderland
Odd One Out
Planet Power
Shaolin Crew

Wachezaji watashindana kwa mfumo wa pointi ambapo kila dau la jumla ya TZS 2,500 litatoa pointi 2. Dau la chini kwa kila mzunguko kwa promosheni hii ni TZS 400.

Kulingana na msimamo wa mwisho, wachezaji 40 watazawadiwa pesa taslimu na mizunguko ya bure kucheza kwenye kasino ya mtandaoni kama ifuatavyo:

Nafasi ya 1 – TSH 2,500,000
Nafasi ya 2 - TSH 1,500,000
Nafasi ya 3 – TSH 500,000
Nafasi ya 4 na 5 - TSH 250,000 kila mmoja
Nafasi ya 6 mpaka 10 – Mizunguko 300 ya bure kwenye sloti ya PIA
Nafasi ya 11 mpaka 20 - Mizunguko 200 ya bure kwenye sloti ya PIA
Nafasi ya 21. mpaka 30 - Mizunguko 100 ya bure kwenye sloti ya PIA
Nafasi ya 31. mpaka 40 - Mizunguko 50 ya bure kwenye sloti ya PIA

Ushindi utakaotokana na Mizunguko ya bure utahitaji kuzungushwa mara 60x (kwa mfano, ukishinda TZS 10,000 kwenye Mizunguko ya bure, utahitaji kucheza TZS 600,000 kwenye mchezo uleule ili kuhamisha ushindi wako kwenye akaunti ya pesa halisi).



Taarifa kuhusu malipo ya juu kwa kila Kundi la Mizunguko ya bure, washindi watapokea taarifa ambayo itatumwa kwao si zaidi ya saa 13:00 AM tarehe 18.05.2024.


Balozi wa bidhaa za taulo za (Baby Cheeky Diaper) mwigizaji Elizabeth Michael maarufu "Lulu" akionesha namna taulo za watoto za (Baby Cheeky Diaper) zinavyofanya kazi kwa kufyonza maji na mtoto kubaki mkavu kabisa.

Balozi wa bidhaa za taulo za (Baby Cheeky Diaper) mwigizaji Elizabeth Michael maarufu "Lulu" akionesha namna taulo za watoto za (Baby Cheeky Diaper) zinavyofanya kazi kwa kufyonza maji na mtoto kubaki mkavu kabisa.

Balozi wa bidhaa za taulo za (Baby Cheeky Diaper) mwigizaji Elizabeth Michael maarufu "Lulu" akikabidhi taulo za taulo (Baby Cheeky, Cuidado na Pinotex) kwa mganga mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke Dr. Joseph Kimaro kulia ni Dkt. Idda Luhanga Mkurugenzi wa Premature Babies Organization.


BALOZI wa bidhaa za taulo za Baby Cheeky Diaper) mwigizaji Elizabeth Michael maarufu "Lulu" amesema bidhaa hizo zina ubora wa hali ya juu na zinafaa kutumiwa na akina mama mara baada ya kujifungua watoto na nyakati zingine zote kwani zinawafanya kuwa wakavu na salama zaidi

Amesema kama vile bidhaa ya Unisex Adult Diaper hii ni suluhisho la ukavu baada ya kujifungua na inaweza kutumiwa na akina mama wote mara baada ya kujifungua kwani ina uwezo na ukavu mara dufu ambapo inafanya kazi nzuri ya ufyonzaji thabiti, kuzuia kuvuja, ulinzi wa muda mrefu na ni mbadala wa (Maternity Pad) .

Elizabeth Michael ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha mradi wa “Diaper Care” ulioanza tarehe29/04/2024 katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke. Mradi ambao una lengo la kumuelimisha mama juu ya matumizi ya taulo za wakubwa (Adult Diapers) kama mbadala wa pedi za uzazi(Maternity Pads)hasa baada ya kujifungua.

Kampuni ya DRAFCO GROUP LTD inahusika na utengenezaji na usambazaji wa taulo (Baby and Adult Diapers) za BABY CHEEKY, CUIDADO na PINOTEX kwa ajili ya matumizi ya watoto wadogo pamoja na akina mama watu wakubwa hapa nchini Tanzania imeamua kutoa elimu hiyo na msaada wa taulo kwa akina mama wanaojifungua na watoto katika hospitali ya rufaa ya Temeke ili kuwapa uelewa wa namna ya kutumia taulo hizo kuwasaidia gharama za uzazi ikiwa ni pamoja na kuwapa furaha wakati wote watumiapo taulo hizo.

Kampuni hii ikiwa chini ya Balozi wake Elizabeth Michael (Lulu) ndiyo waliowezesha mradi huu kwa kugharamia utoaji elimu, misaada kwa wahitaji na kuhakikisha usambazaji na upatikanaji wa taulo hizi unawafikia walengwa na wahitaji nchi nzima.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Temeke Dr. Joseph Kimaro ameipongeza kampuni ya DRAFCO GROUP LTD kwa kutoa elimu pamoja na kugawa taulo za watoto na wanawake kwa wahitaji katika hospitali ya Temeke zenye thamani ya shilingi milioni 16.

"Tunashukuru kwa kuwa tumepewa Diaper kwa ajili ya watoto wachanaga na watu wazima jambo hili mlilofanya ni jambo la kujitolea na ni sadaka",amesema Dr. Kimaro.

Amesema Serikali inahimiza watu binafsi mashirika na makampuni kusaidia ili kuhakikisha sekta ya afya inaimarika na kugusa maisha ya watu.

Amesema ugawaji wa tauli hizo umesaidia wahitaji wengi lakini umechangia katika sekta ya afya kwenye kuboresha afya za wananchi.

Ameongeza kuwa siku tano za kazi ya kutoa elimu iliyofanyika hospital hapo wameweza kuwafiki akina mama 1500 ambapo watu hao nao wanaweza kupeleka elimu kwa wengine.

"Tunaamini watu zaid ya 15000 watakuwa wamepata elimu kuhusu hizi bidhaa kazi kubwa mmeifanya na sisi tutaendelea kuunga mkono juhudi zenu kwa kufanya tafiti katika hizi bidhaa za taulo za wakubwa",amesema.

Ameongeza kuwa wataenda kufanya tafiti na kuangali kama wataweza kupima wingi wa damu iliyopotea wakati mama anapojifungua kama kitaendana na kipimo cha kimaabara na kusaidia katika kazi nzima ta tiba kwa akina mama.

Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Temeke Dr. Joseph Kimaro akionesha moja ya picha inayoonesha mtoto njiti.


Dkt. Idda Luhanga Mkurugenzi wa Premature Babies Organization akizungumza wakati wa makabidhiano hayo.

Na Munir Shemweta, MLELE

Mkazi wa kijiji cha Luchima katika kata ya Majimoto halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile ametoa shilingi elfu tano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi.

Kiasi hicho cha pesa kimekabidhiwa kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda tarehe 3 Mei 2024 wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Luchima alipokwenda kuzungumza nao wakati wa ziara yake ya kuwafariji wananchi waliopatwa na mafuriko katika jimbo lake la Kavuu.

‘’Nampongeza rais kwa vitendo kabisa naomba mhe, mbunge leo nikikabidhiwa fedha taslimu shilingi elfu tano umpelelekee Mhe, Rais ’’ alisema.

Kwa mujibu wa mwananchi huyo, uamuzi wake unatokana na kuwiwa na uongozi bora na utendaji kazi wa Rais Samia hasa kwa kuwajali wananchi wa Luchima ambapo mbali na mambo mengine amewajali kwa kutoa fedha milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati aliyoieleza imewakomboa wananchi wa kijiji hicho.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda amesema atahakikisha kiasi hicho cha fedha kilichotolewa na mwananchi huyo kinamfikia mhe, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Amempongeza mwananchi huyo wa kijiji cha Luchima wa uamuzi wake wa kutoa kiasi hicho cha fedha kama ishara ya kukubali juhudi na kazi kubwa inayofanywa na Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Luchima na Tanzania kwa ujumla.

Amewaaleleza wananchi wa kijiji hicho kuwa, Rais Samia anawapenda sana na amekuwa akisaidia juhudi mbalimbali za maendeleo kwenye jimbo la Kavuu na kutaja baadhi ya juhudi hizo kuwa ni pamoja na kutoa fedha za ujenzi wa hospitali, shule, barabara pamoja na upatikanaji wa huduma za maji.

Mhe, Pinda amefanya ziara katika jimbo lake la Kavuu kuwafariji wananchi waliopatwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa na kuathiri miundiombinu ikiwemo madaraja.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda akimpongeza mkazi wa kijiji cha Luchima katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile aliyetoa shilingi elfu tano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi tarehe 2 Mei 2024.
Mkazi wa kijiji cha Luchima katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile akizungumza mara baada ya kumkabidhi shilingi elfu tano Naibu Waziri wa Ardhi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda aliyoitoa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi tarehe 3 Mei 2024.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya  Makazi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda akimpongeza mkazi wa kijiji cha Luchima katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile aliyetoa shilingi elfu tano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi tarehe 2 Mei 2024.

Na Mwandishi Wetu

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limepokea taarifa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kuhusu uwepo wa kimbunga “HIDAYA” katika Bahari ya Hindi mashariki mwa pwani ya nchi yetu.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC ilisema Kimbunga “HIDAYA” kimeendelea kuimarika na kusogea kuelekea maeneo ya pwani ya nchi yetu ambapo hadi kufika saa tisa usiku wa tarehe 03 Mei 2024 kilikuwa kimeimarika zaidina kufikia hadhi ya Kimbunga kamili kikiwa umbali wa takriban Kilomita 401 mashariki mwa pwani ya Mtwara.

Aidha taarifa hiyo ilisema tangu wakati huo,kimbunga HIDAYA kimeendelea kuimarika zaidi huku kasi ya upepo ikiongezeka hadi kufikia
Kilomita 130 kwa saa. 


TASAC inawataarifu wadau wote wa usafiri kwa njia ya maji kuwa mwenendo wa mifumo  ya hali ya hewa baharini bado unaonesha uwezekano mkubwa wa Kimbunga “HIDAYA”  kusalia katika hadhi ya Kimbunga kamili kwa saa 12 zijazo huku kikiimarika, na kendelea kusogea karibu kabisa na pwani ya Tanzania.

Hata hivyo taarifa ilisema Kimbunga hikikinatarajiwa kuendelea kuwepo hadi tarehe 06 mwezi Mei 2024 na kupungua nguvu baada ya tarehe 6 Mei 2024.

Uwepo wa kimbunga hicho utasababisha ongezeko la mvua na upepo mkali utakaoambatana na mawimbi makubwa baharini yatakayosambaa katika eneo kubwa la mwambao wa bahari yetu.

Kwa msingi huo, TASAC inatoa wito kwa wadau wote wanaofanya shughuli za kiuchumi, wakiwemo wavuvi,kuchukua tahadhari na kujiepusha kufanya shughuli hizo baharini hadi hapo kimbunga kitakapopita katika mwambao wa bahari yetu. 

Kwa vyombo vinavyofanya shughuli za usafirishaji abiria,tunawaasa kuchukua tahadhari kubwa na kutumia taarifa
za hali ya hewa kabla ya kuanza safari.

Aidha TASAC imewaasa wananchi kwa ujumla kujiepusha na shughuli za starehe katika mwambao wa bahari hadi hapo kimbunga kitakapopita katika mwambao wa bahari yetu.

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Daniel Sillo amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Haki, weledi na uadilifu na kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika.

Mhe. Sillo amesema hayo wakati alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Jijini Dodoma na kuzungumza na Makamisha na Maofisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi ikiwa ni mara ya kwanza kutembelea Jeshi la Polisi tangu alipoteuliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Aprili 4,2024.

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura amesema kuwa, Jeshi la Polisi limeendelea kutekeleza makujukumu yake kwa weledi na uadilifu katika kuhakikisha shughuli za kila siku za Jeshi hilo zinaendelea kufanyika kwa kutoa huduma bora na zenye viwango kwa wananchi.






Mawaziri wanaosimamia Sekta ya Afya katika Nchi Wanachama wa Jumuiya Afrika Mashariki wameweka mikakati na kukubaliana kuongeza ushirikiano zaidi katika kuboresha utoaji wa huduma katika sekta hiyo.

Azma hiyo imefikiwa leo tarehe 3 Mei 2024 kwenye Mkutano wa Kawaida wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Afya la Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mawaziri hao wamekutana kwa lengo la kufanya mapitio na maboresho ya mikakati itakayosaidia kutatua chanagamoto zinazo changia kuzorota kwa ustawi wa sekta ya afya katika Jumuiya.

Sambamba na kufikia azima hiyo Mawaziri hao wamekubaliana kufanya kazi kwa pamoja katika kuimarisha mifumo na miundombinu ya utoaji wa huduma za afya ikiwemo uimarishaji wa maabara, maboresho ya programu mbalimbali za afya, maboresho ya mafunzo kwa wataalam wa afya, maboresha ya sera za afya, utafiti na ufuatiliaji.

Vilevile wamejadili na kuweka mikakati makususi ya kukabiliana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari na shinikizo la juu la damu. Mikakati hiyo ni pamoja na kuwashauri na kuwahamasisha wananchi uzingatiaji wa mlo kamili, ufanyaji mazoezi na kuacha au kupunguza matumizi wa pombe.\

Akizungumza katika mkutano huo Waziri wa Afya nchini Mhe. Ummy Mwalimu ameeleza kuwa Tanzania inaendelea na utekelezaji wa mikakati hiyo, ambapo amebainisha kuwa katika suala la uhamasishaji wa ufanyaji mazoezi Serikali imechukua hatua ya kufunga daraja la Tanzanite la jijini Dar es Salaam kwa kila Jumamosi ili kuruhusu wananchi wa kufanya mazoezi katika daraja hilo.

Vilevile Waziri Ummy ametoa wito kwa Baraza hilo kukubali na kupitisha endekezo la Tanzania la kuanzisha Kituo cha Umahiri cha Upandikizaji Uloto (kwa wototo wenye sickle Cell) na Sayansi ya Matibabu ya Magonjwa ya Damu chini ya Hospitali ya Benjamin Mkapa na Kituo cha Umahiri cha Sayansi ya Afya ya Kinywa chini ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)

Mbali na hayo Mawaziri hao wamejadili kuhusu namna ya kubaliana na changamoto mbalimbali zinazochangia kuzorota kwa sekta hiyo katika Jumuiya. Wamezita changamoto hizo kuwa ni pamoja na Mabaliko ya Tabia Nchi, uhaba wa fedha za kuendesha programu na miradi mbalimbali ya afya, milipuko ya magonjwa, kuzuka kwa vita na mapigano kwenye baadhi ya maeneo katika Jumuiya, uhaba wa wataalam na miundombinu isiyotosheleza mahitaji ikiwemo vituo vya afya na vifaa tiba.

Katika kukabiliana na changamoto hizo wamepitisha mikakati kadhaa ya kukabiliana nazo ikiwemo; kupishwa ni kuimarisha mfumo wa ununuzi wa dawa kwa pamoja, kupitisha mpango mkakati wa pamoja wa masuala ya afya wa Jumuiya kwa mwaka 2024 hadi 30, kuimarisha ufuatiliaji na utambuzi wa wagonjwa, kukamilisha na kuwasilisha andiko la kuomba fedha za kukabiliana na majanga, kuimarisha afua za kinga ili kutokomeza malaria katika Jumuiya na kuendelea kusimamia Vyuo Vikuu vya Afya ili viendelee kutoa elimu bora ndani ya Jumuiya.

Mkutano huo uliofanyika kwa siku tano kuanzia terehe 29 Aprili hadi tarehe 3 Mei 2024 uliaanza katika Ngazi ya Wataalam ambapo pamoja na masuala mengine walikufanya tathimini ya utekelezaji wa maagizo na makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa 23 wa Baraza hilo. Tarehe 2 Aprili 2024 uliendelea katika Ngazi ya Makatibu Wakuu na kuhitimishwa na Mkutano wa Mawaziri tarehe 3 Mei 2024.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akichangia mada kwenye Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Afya wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mei 3, 2024.
Mawaziri na Makatibu Wakuu wanaosimamia Sekta ya Afya katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania wakifuatilia Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Afya wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mei 3, 2024.
Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Afya wa Afrika Mashariki ukiendelea.

IJUMAA ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet tayari wamekuwekea ODDDS za kibabe na machaguo zaidi ya 1000. Ingia meridianbet na usuke mkeka wako hapa.

EPL leo hii kutakuwa na mechi moja ambayo Luton Town atakuwa mwenyeji wa Everton ambao wametoka kushinda mechi yao iliyopita. Mwenyeji anahitaji pointi tatu leo ili ajiweke kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa ligi. Meridianbet wamempa The Toffees nafasi kubwa ya kushinda mechi hii kwa ODDS 2.55 kwa 2.60. Beti sasa.

Ligi kuu nyingine ambayo leo hii itaendelea ni kule Hispania yaani LALIGA mechi moja ya Getafe dhidi ya Athletic Club ambao wapo nafasi ya tano kwenye ligi. Mechi hiyo itapigwa kwenye dimba la Coliseum huku mechi ya mwisho walipokurtana walitoshana nguvu. Mechi hii imepewa ODDS 3.57 kwa 2.16. Jisajili hapa.

Ukiachana na mechi ndugu mteja kumbuka kucheza michezo ya Kasino ya Mtandaoni ambayo inatolewa ndani ya meridianbet kama vile Poker, Roullette, Aviator, Rockertman, Keno, Sloti na mingine kibao. Ingia mchezoni na ucheze sasa.

Lakini vilevile BUNDESLIGA nayo itarindima ambapo RB Leipzig baada ya kushinda mechi yake iliyopita, leo hii atakuwa ugenini kusaka pointi tatu dhidi ya TSG Hoffenheim. Mwenyeji ametoka kupoteza mchezo wake uliopita huku ndani ya Meridianbet anayependelewa zaidi kuondoka na pointi tatu ni RB akiwa na ODDS 1.47 kwa 5.48.

Halikadhalika SERIE A leo hii itakuwa mzigoni saa 3:45 Torino atapepetana dhidi ya Bologna ambao wamekuwa na kiwango kizuri sana msimu huu. Mwenyeji yupo nafasi ya 10 na mgeni yupo nafasi ya 4. Tofauti ya pointi kati yao ni 17. Je nani kuibuka kidedea? Bashiri mechi hii sasa. Ikiwa imepewa ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000.

LIGUE 1 kule Ufaransa kuna mechi ya kibabe kabisa Toulouse uso kwa uso dhidi ya Montpellier ambao wametoka kutoa sare mechi yao iliyopita. Mwenyeji yeye aliondoka na ushindi. Mechi ya mkondo wa kwanza kukutana, Mgeni alishinda. Je leo hii Toulouse atalipa kisasi?. Beti mechi hii sasa.

Mechi nyingine itakuwa majira ya saa 4:00 usiku ambapo RC Lens baada ya kupoteza mechi iliyopita, leo atakuwa nyumbani kuzichabanga dhidi ya FC Lorient ambao wapo nafasi ya pili kutoka mwisho kwenye ligi. Meridianbet wamempa mwenyeji nafasi ya kushinda kwa ODDS 1.39 kwa 7.05. Nani kushinda leo huku mechi ya kwanza walipokutana walitoshana nguvu.?
--Awahimiza Wachungaji kuwa na Maono Makubwa
--Awataka kuhubiri amani na upendo
--Awahimiza kumtia moyo Rais Samia kutekeleza miradi ya maendeleo

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewashauri wachungaji kuwa na maono makubwa katika kuongoza waumini katika makanisa yao ili kujenga Taifa la watu wenye mwelekeo chanya.

Akizungumza leo (Mei 3, 2024) Jijini Dodoma wakati wa kufunga kikao cha mazungativu (Retreat) kwa wachungaji wa Kanisa la FPCT, Dkt. Biteko amesema kuwa ili waumini wapate uelekeo wa kwenda mahali fulani, wanahitaji mtu mmoja miongoni mwao atakaye waongoza kufikia malengo waliyojiwekea kutokana na maono aliyonayo.

“Wachungaji msihangaike na wingi wa watu mahali popote, angalia uwezo wa kiongozi anayeona mbali atawaongoza wafike mbali”, amesema Dkt. Biteko.

Ameongeza kuwa “ Askofu Mkuu umechagua fungu jema kufanya wachungaji hawa wakutane hapa kujiongezea maarifa kwa kuwa tuko katika dunia iliyojaa utandawazi na mafundisho ya kweli na yasiyo ya kweli. Ni vigumu kwa waumini kutambua ya kweli na yasiyo ya kweli hivyo, wanahitaji kuongozwa”.

Aidha, Dkt. Biteko amewahimiza viongozi wa dini kuwaongoza waumini kiroho na kuchagua viongozi sahihi wanaofahamu kuwa watawaletea maendeleo na ustawi wa nchi.

Pia, amewaomba viongozi wa dini kuwahimiza waumini kufanya kazi kwa bidii, kuhubiri kuhusu amani pamoja na kusisitiza maadili kwa waumini.

Dkt. Biteko ametaja mafanikio mbalimbali ya Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, huku akiwaomba wachungaji hao kuendelea kumuombea na kumtia moyo ili aendelee kutekeleza miradi ya nchi katika maeneo mbalimbali.

“ Mradi wa reli ya kisasa (SGR) ni mradi mkubwa haikuwa rahisi kupata fedha za kutekeleza mradi huu lakini Rais Samia amefanikiwa, Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere unaozalisha megawati 2115 umefanikiwa, Pia Serikali imejenga madarasa, zahanati, vituo vya afya na kutoa ajira kwa watumishi wa sekta ya afya, angalieni nia yake, muungeni mkono”, amebainisha Dkt. Biteko.

Vilevile, amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa dini na imani za watu hivyo viongozi wa dini wahimize waumini kuchagua viongozi wanaofaa

“Mwaka huu tuna uchaguzi wa Serikali za Mitaa, viongozi wa dini mna uwezo wa kuwahamasisha waumini waweze kuchagua viongozi wanaowahitaji kwa ajili ya kuwaletea maendeleo”, amesisitiza Dkt. Biteko.

Naye, Askofu Mkuu wa FPCT, Steven Mulenga amesema kuwa lengo la semina hiyo ya siku nne kwa wachungaji ni kuwajengea uwezo watumishi wa Mungu namna ya kumkaribisha Yesu Kristo.

“ Haya tuliyofundishana yatakuwa na matokeo kwa nchi ya Tanzania”, amesema Askofu Mulenga.

Semina hiyo wa wachungaji FPCT imehudhuriwa na wachungaji kutoka nchi za Kenya, DRC, Rwanda na Sudani Kusini.






NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wafanyabishara wa bidhaa za vipodozi kuhakikisha wanasajili bidhaa zao , kuthibitisha ubora wake pamoja na kusajili maeneo yanayohusika na uzalishaji, uuzaji na uhifadhi kwa mujibu wa matakwa ya sheria ya viwango Sura ya 130 ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

Wito huo umetolewa leo Mei 3, 2024 Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya wakati akifungua Kikao baina ya TBS na wazalishaji, waagizaji na wasambazaji wa bidhaa za vipodozi nchini.

"Madhara ya kiafya yanayoweza kusababishwa na matumizi ya vipodozi vyenye viambata sumu ni pamoja na saratani ya ngozi, kuathiri mfumo wa uzazi, kuathiri figo, kuathiri afya ya ngozi na kusababisha ngozi kushindwa kuhimili joto pamoja na kushambuliwa kirahisi na magonjwa ya ngozi". Amesema Dkt. Ngenya.

Aidha Dkt. Ngenya amesema katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2022/2023 hadi mwezi Aprili 2024, wamekamata na kuharibu vipodozi vyenye viambata sumu vinavyokadiriwa kuwa na uzito wa tani 114 na thamani ya shilingi bilioni 1.49.

Amesema kuwa Shirika litaendelea kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa wale watakaoendelea kukiuka matakwa ya sheria katika uuzaji wa vipodozi.

Amesema wafanyabiashara hao wa vipodozi wanapaswa kuhakikisha wanazalisha na kusambaza bidhaa za vipodozi vilivyokidhi matakwa vya viwango ili visiweze kusababisha madhara ya kiafya kwa watumiaji wa bidhaa hizo.











Top News